Tuesday, 28 September 2021

R.KELLY APATIKANA NA HATIA

 


Mwimbaji wa nyimbo za R&B Mmarekani , R .Kelly amepatikana na hatia ya biashara ya ngono na unyanyasaji ambayo amekuwa akishutumiwa kwa muda mrefu 

Msanii huyo amekuwa rumande kwa majaribio baada ya kushukiwa tangu mwaka wa 2019 kwa makosa 14 ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia ,utekaji nyara ,rushwa , na biashara ya ngono .Vilevile amehukumiwa na makosa mengine manane ikiwemo ukiukaji was sheria ya Mann  , ukiukaji wa sheria ya biashara ya ngono (usafirishaji wa binadamu kwa mudhumuni mabaya)

Japokuwa ,R.Kelly ambaye anajulikana kwa nyimbo kama vile "I believe I can fly , Sign of  a Victory "alikana madai hayo akisaidiwa na Mwanasheria wake wakipingana na mashahidi takriban sita walikuwa wakisema kuwa Mwimbaji huyo alikuwa mviziaji aliyekuwa akinyanyasa wasichana wenye umri mdogo kingono.


Waendeshaji mashtaka wa Shirikisho katika Wilaya ya Mashariki ya New York walifanikiwa kudhibitisha tuhuma hizo kupitia kwa wanaume saba na wasichana watano kuwa R .Kelly ni kiongozi wa uhuni ambapo madhumuni yake ilikuwa kushawishi vijana wadogo wa kiume na like na hata wan awake katika ajenda zake mbovu .

Kutokana na tuhuma izo, amepatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka kumi .Kifungo chake kitaanza Mwezi Mei, 4 , 2022 .


Wednesday, 8 September 2021

Klean Heart apania siasani

 

Mkongwe wa muziki na pia CEO wa Pillar Works studios aweka wazi azma yake ya kuwania kiti cha Udiwani (MCA) mjini Malindi mwaka wa 2022 .
Mashabiki wake wamedhibitisha hilo baada ya posti zake za hivi karibuni katika kurasa zake za mitandao ya kijamii .Je atawezana na ushindani uliopo mjini Malindi  ama anajipotezea muda ?Na je akipata nafasi ataweza kumudu sekta zote mbili kwa ukamilifu(muziki na siasa )? 
Tunamfuatilia mkongwe huyu wa muziki kujua ukweli kuhusu madai haya.


Monday, 26 July 2021

USHAURI NASAHA

Kila mtu anatamani siku moja aje kuwa na maisha mazuri , kila mmoja anatamani awe mtu kati ya watu , asimame siku moja na kujivunia mali alizozipata kupitia juhudi zake, asimame na kusema hiki ni kwa sababu ya bidii zangu za usiku na mchana.Namaanisha , kila mmoja ana ndoto ya kuwa mtu flani mbeleni 

Mali humfanya mtu kuheshimiwa miongoni mwa watu , humfanya mtu kuombwa ushauri panapokuwa na mashauri mahala popote pale . Lakini pia mali hiyo haiwezi kuja bila juhudi . Mali ipatikanayo bila juhudi haiishi maswali . Mali ya urithi kuitumia kwa 

Google courtesy 


umakini kama mali uliyoipata kwa jasho lako mwenyewe 

Katika utafutaji wa maisha mazuri , mtu hupitia misukosuko mingi ikiwemo kudharauliwa , kutolewa maana , kutoaminiwa katika uwezo wako na hata kuchekwa ,yote haya kukufanya kuvunjika moyo na kusitisha safari yako uliyoipanga ya kimaisha . Mambo haya yanaweza kuvunja moyo kwelikweli sio masiara lakini vilevile mambo haya ukiyaangalia katika mtazamo chanya , yanaweza kukufanya ukaendelea kusukuma gurudumu lako na kuhakikisha maisha yako yanakuwa mazuri siku za usoni .

Mtu anayekusema inamaana kwamba kunao uwezo ulionao wewe ambao yeye hana ila anafanya hivyo kusudi ili kukuvuruga akili na kukuvunja moyo  

Kila mtu anabahati yake katika maisha , juhudi ndio funguo ya kugundua pale bahati yako ilipo , Cha msingi piga juhudi zako ufungue bahati yako 

Google courtesy