Kila mtu anatamani siku moja aje kuwa na maisha mazuri , kila mmoja anatamani awe mtu kati ya watu , asimame siku moja na kujivunia mali alizozipata kupitia juhudi zake, asimame na kusema hiki ni kwa sababu ya bidii zangu za usiku na mchana.Namaanisha , kila mmoja ana ndoto ya kuwa mtu flani mbeleni
Mali humfanya mtu kuheshimiwa miongoni mwa watu , humfanya mtu kuombwa ushauri panapokuwa na mashauri mahala popote pale . Lakini pia mali hiyo haiwezi kuja bila juhudi . Mali ipatikanayo bila juhudi haiishi maswali . Mali ya urithi kuitumia kwa
![]() |
| Google courtesy |
umakini kama mali uliyoipata kwa jasho lako mwenyewe
Katika utafutaji wa maisha mazuri , mtu hupitia misukosuko mingi ikiwemo kudharauliwa , kutolewa maana , kutoaminiwa katika uwezo wako na hata kuchekwa ,yote haya kukufanya kuvunjika moyo na kusitisha safari yako uliyoipanga ya kimaisha . Mambo haya yanaweza kuvunja moyo kwelikweli sio masiara lakini vilevile mambo haya ukiyaangalia katika mtazamo chanya , yanaweza kukufanya ukaendelea kusukuma gurudumu lako na kuhakikisha maisha yako yanakuwa mazuri siku za usoni .
Mtu anayekusema inamaana kwamba kunao uwezo ulionao wewe ambao yeye hana ila anafanya hivyo kusudi ili kukuvuruga akili na kukuvunja moyo
Kila mtu anabahati yake katika maisha , juhudi ndio funguo ya kugundua pale bahati yako ilipo , Cha msingi piga juhudi zako ufungue bahati yako
![]() |
| Google courtesy |


No comments:
Post a Comment