Mwimbaji wa nyimbo za R&B Mmarekani , R .Kelly amepatikana na hatia ya biashara ya ngono na unyanyasaji ambayo amekuwa akishutumiwa kwa muda mrefu
Msanii huyo amekuwa rumande kwa majaribio baada ya kushukiwa tangu mwaka wa 2019 kwa makosa 14 ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia ,utekaji nyara ,rushwa , na biashara ya ngono .Vilevile amehukumiwa na makosa mengine manane ikiwemo ukiukaji was sheria ya Mann , ukiukaji wa sheria ya biashara ya ngono (usafirishaji wa binadamu kwa mudhumuni mabaya)
Japokuwa ,R.Kelly ambaye anajulikana kwa nyimbo kama vile "I believe I can fly , Sign of a Victory "alikana madai hayo akisaidiwa na Mwanasheria wake wakipingana na mashahidi takriban sita walikuwa wakisema kuwa Mwimbaji huyo alikuwa mviziaji aliyekuwa akinyanyasa wasichana wenye umri mdogo kingono.
Waendeshaji mashtaka wa Shirikisho katika Wilaya ya Mashariki ya New York walifanikiwa kudhibitisha tuhuma hizo kupitia kwa wanaume saba na wasichana watano kuwa R .Kelly ni kiongozi wa uhuni ambapo madhumuni yake ilikuwa kushawishi vijana wadogo wa kiume na like na hata wan awake katika ajenda zake mbovu .
Kutokana na tuhuma izo, amepatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka kumi .Kifungo chake kitaanza Mwezi Mei, 4 , 2022 .


Nice piece Kaka..
ReplyDelete